Papa awasalia wanafunzi waliouawa Kenya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa francis akisali

Papa Francis amewasalia hadharani wanafunzi wa Kenya waliouwawa Alhamisi.

Akitoa ujumbe wake wa pasaka mbele ya umati mkubwa katika medani ya Saint Peter's, Vatican, Papa Francis alitoa wito kwa mateso dhidi ya Wakristo dunia nzima kukomeshwa.

Kiongozi huyo wa kidini anayewaongoza karibia wafuasi billioni 1.2 wa kanisa katoliki alipinga yale yanayoendelea mashariki ya kati na kwengineko lakini akitumai kwamba makubaliano ya mpango wa nyuklia nchini Iran ni hatua muhimu ya kuimarisha usalama duniani.

Kabla ya kuanza mahubiri yake, Papa alikwenda kwenye medani kuwalaki watu waliofika hapo ingawa mvua ikinyesha.