UN yaomba vita visitishwe Yarmouk

Haki miliki ya picha
Image caption kambi ya wakimbizi ya yarmouk nchini Syria

Umoja wa mataifa umetoa wito wa ghasia zimalizwe katika eneo la Yarmouk, kambi ya Wapalestina mjini Damascus, ili kuruhusu raia waondolewe.

Eneo hilo kwa jumla sasa linadhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State, ambao wanapambana na wanamgambo wa Kipalestina.

Yarmouk ni mahala ambapo tayari wanawake wanakufa wanapoji-fungua kwa kukosa dawa, huku watoto pia wakifariki kutokana na njaa.

Sasa mapambano makali yanaendelea barabarani, watu wamejificha majumbani mwao wakiogopa kwenda popote.