Akon awajibu wanamuziki wa Kenya

Image caption Mwanamuziki wa Marekani Akon

Mwanamuziki mwenye tuzo la kimataifa Akon amesema kuwa hakuna hata mwanamuziki mmoja wa Kenya ambaye amemuomba kufanya naye 'kolabo'mara zote tano ambazo ameweza kuzuru Kenya.

Akon Hatahivyo ameliambia jarida la Mondayblues nchini Kenya kwamba wasanii wa muziki barani Afrika pia wanafaa kuimarisha viwango vyao ili kutoa changomoto kwa wasanii kama yeye ili kuweza kushirikiana nao.

Tamko la msanii huyo linajiri kufuatia madai kutoka kwa wanamuziki wa Kenya kwamba hayuko tayari kufanya nao Kazi.