Rand Paul atangaza nia Marekani

Image caption Rand Paul seneta wa Kentucky

Seneta kutoka Kentucky wa chama cha Republican Rand Paul, ametangaza nia rasmi, kuwa atagombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani.

Paul ameyasema hayo wakati wa kampeni zake anazoziendesha kupitia tovuti yake, na amenukuliwa kuwa anataka kuirejesha nchi hiyo katika kanuni uhuru na serikali ndogo.

Kampeni zake alizindulia katika jimbo la Louisville mapema wiki hii. Rand Paul ameungana na seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz, katika harakati hizo ambazo zimevuta hisia za nusu ya wagombea wakubwa wa chama cha Republican,na hii ni pamoja na gavana wa zamani wa jimbo la Florida Jeb Bush,gavana wa Wesconsin Scott Walker,ambaye bado hajatoa tamko lake rasmi .