Waziri mkuu wa Ugiriki kukutana na Putin

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, amewasili mjini Moscow kukutana Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo maalum.

Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, amewasili mjini Moscow kukutana rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo maalum.

Ugiriki inasema kuwa mazungumzo yao yatajadili uhusiano kati ya muungano wa bara Ulaya na Urusi.

Uhusiano huo ulidorora kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi punde kufuatia mzozo wa Ukraine.

Wachanganuzi wanasema kuwa Athens inapania kuboresha uhusiano na Moscow hasa ikiwa uhusiano wao na wadeni wao bara Ulaya wa kuikopesha pesa ukishindwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ugiriki inafaa kulipa deni la dola milioni 886 kwa shirika la fedha duniani IMF hapo kesho Alhamisi.

Ugiriki inafaa kulipa deni la dola milioni 886 kwa shirika la fedha duniani IMF hapo kesho alhamisi.

Mwandishi wa BBC aliyeko jijini Moscow anasema kuwa Ugiriki inataka kutumia mkutano huo jijini Moscow

ili kuwaonyesha washirika wake wanaoipa mkopo kuwa ina njia mbadala ya kupata msaada wa kifedha, lakini ukweli ni kwamba inataka jumuia ya bara Ulaya kuiondolea madeni yanayoisakama.