Harakati za makundi ya kigaidi zasababisha akaunti nane za watu binafsi kufungwa nchini Kenya.
Huwezi kusikiliza tena

Al Shabaab Akaunt 86 zafungwa Kenya

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Joseph Nkaissery, ameithibitishia BBC kwamba serikali ya Kenya imesitisha matumizi ya akaunti za watu

binafsi wapatao 86 wanaoshukiwa kuhusika na ufadhili wa kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini humo.

Akaunti za watu hao ambao zimesitishwa ni baadhi ya watu waliokuwa katika orodha ya serikali ya Kenya ambao walikuwa wakifuatiliwa mienendo yao.

Makampuni 13 za ubadilishaji na usafirishaji wa fedha nazo zimefungwa.

Serikali ya Kenya imetoa ushauri kwa wateja wa mabenki wa madhehebu ya dini ya kiislamu kutumia akaunti za benki za Sharia ambazo zimethibitishwa na benki kuu ya Kenya.

Msemaji wa muungano wa wanaosafirisha fedha kwa njia ambayo inajulikana kama Hawala ambao nao pia wamezuiwa

Abdi Ali anasema wako makini na uamuzi huo na kwamba tayari wamewaagiza wanasheria wao kushughulikia hali hiyo.