Yemen:Houthi yakamia mji wa Aden

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapiganaji Yemen wanakamia Aden

Wapiganaji waasi nchini Yemen wamezidisha mapigano yao katika hatua za kuuthibiti kabisa mji wa Aden.

Nyumba kadhaa zimechomwa moto huku sauti zikisikika kutoka kwenye vipaza sauti misikitini,

ya kuwataka raia wote wa mji huo kujitokeza ili kutetea mji wao usitwaliwe na waasi.

Wakati huo huo, kuna ripoti kuwaege za muungano zikiongozwa na majeshi ya Saudi Arabia zinazounga mkono

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani ilisema kuwa inaharakisha kuwasilisha silaha kwa majeshi ya muungano

serikali ya Yemen, yakirusha mabomu katika ngome ya waasi katika viunga vya mji wa Aden upande wa kazkazini.

Awali Marekani ilisema kuwa inaharakisha kuwasilisha silaha kwa majeshi ya muungano, yanayoongozwa na Saudi Arabia,

katika makabiliano dhidi ya kundi la waasi wa Kishia la Houthi, nchini Yemen.

Awali hali ya taharuki ilitanda kote katika mji huo wa pwani baada ya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iran imezua taharuki baada ya kutuma Manuari yake katika bahari ya Yemen

Iran Kutuma manuari mbili za kivita katika bahari inayopakana na eneo la Aden nchini Yemen.

Kamanda mmoja wa jeshi la Iran amesema manuwari hizo zimetumwa katika eneo hilo kulinda taifa lake kutokana na uharamia.

Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa hatua hiyo huenda ikachochea uhasama zaidi katika eneo hilo.

Saudi Arabia inaongoza jeshi la muungano linalokabiliana na wapiganaji wa kiislamu wa kishia nchini Yemen, wapiganaji ambao wanakisiwa kupewa misaada na utawala wa Tehran.