Kanye West aomba Msamaha

Image caption Kanye West aomba Msamaha

Kanye West ametekeleza matakwa ya kesi iliyokuwa ikimkabilia ya kumpiga paparazi.

Paparazi huyo alimtaka West kukutana naye palepale alipompiga na kumuomba msamaha na kisha salamu.

Sasa picha zimeibuka zikionesha mwanamuziki huyo wa mdundo wa kufoka akitabasamu na paparazi aliyemshtaki.

Mpiga picha wa magazeti ya umbea Daniel Ramos alimshtaki West kwa kumshambulia baada ya kumuuliza kwanini alikuwa anasusia maswali ya waandishi wa habari nje ya uwanja wa Los Angeles..

Wakili wake ,Gloria Allred amesema kuwa wawili hao walikutana na West akaomba msamaha.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kanye West ametekeleza matakwa ya kesi iliyokuwa ikimkabilia ya kumpiga paparazi.

Hata hivyo vipengee mahsusi ya makubaliano hayo na msamaha hayajabainika.

Kwa upande wake wakili anayemwakilisha bwana West ,Shawn Holley, amenyamaza kimya!

West, 37, aliomba mahakama imuonee huruma kwa kosa hilo la kumvamia mtu.

West anachunguzwa.