Viongozi wa kiislamu wazuru Garissa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wa kiislamu wazuru eneo la Garissa

Viongozi kadhaa wa kiislamu nchini Kenya wanazuru mji wa mashariki wa Garissa ambapo wiki ilopita watu 148 waliuawa katika chuo kikuu na wapiganaji wa kundi la Alshabaab.

Wanajadiliana kuhusu vile wanavyoweza kumaliza makundi yenye misimamo mikali.

Wabunge hao na wanachama wa makundi ya kidini katika eneo hilo pia wataitembelea miji ya kazkazini mashariki kama vile Wajir na Mandera ambayo pia imeathiriwa vibaya na mashambulizi ya Al Shabaab.