Maduro aitaka Marekani kuondoa vikwazo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Venezuela Nicholas Maduro

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema kuwa anampelekea barua rais wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano wa nchi za Amerika nchini panama yenye sahihi za zaidi ya watu milioni kumi raia wa Venezuela.

Barua hiyo inataka kundolewa kwa vikwazo vilivyotangazwa na Marekani dhidi ya maafisa kadha nchini Venezuela wiki tatu zilizopita.

Marekani inawashutumu maafisa hao kwa kuendesha vitendo vinavyokiuka haki za binadamu dhidi ya wapinzani wa rais Maduro. Bwana Maduro amesema kuwa matamshi ya hivi majuzi ya rais Obama kuwa Venezuela si tisho kwa Marekani yatasaidia kufungua awamu mpya ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwandishi mwa BBC aliyeko nchini Venezula anasema kuwa vikwazo hivyo vimesababisha kuwepo uhaba wa bidhaa muhimu huku milolongo mirefu ya watu ikiwa jambo la kawaida kwenye mji mkuu Caracas.