Obama na Castro wakutana Panama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Panama kushoto,Raul Castro wa Cuba katikati na Barrack Obama wa Marekani kulia

Marais wa Marekani na Cuba wameamkuana kwa mikono na kuzungumza kwa muda mfupi wakati wa kuanza kwa mkutano wa nchi za Amerika ambayo ni ishara ya uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Rais Obama na mwenzake RaulCastro wanatarajiwa kuwa na mazungumzo ya kihistoria nchini Panama leo jumamosi ambayo ni mazungumzo ya kwanza ya aina hiyo kati ya viongozi wa Marekani na Cuba kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Mapema rais Obama alisema kuwa Marekani inafungua ukurasa mpya wa uhusiano kati yake na Cuba na ana matumaini kuwa utasaida watu wa Cuba kufanya uamuzi wao siku za usoni.