Wakimbizi wa Somalia:Kenya yaonya UN

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi wa Somalia katika kambi ya wakimbizi wa Daadab nchini Kenya

Serikali ya Kenya imeupatia Umoja wa Mataifa makataa ya miezi mitatu kuwahamisha wakimbizi wa Somalia wapatao nusu milioni hadi nchini Somalia.

Naibu rais William Ruto amesema kuwa iwapo Umoja wa mataifa utakataa kuwahamisha wakimbizi hao, Kenya itachukua jukumu la kuwandoa.

Makataa hayo yanajiri siku kadhaa baada ya shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 148 waliuawa na kundi la wapiganaji wa Al-shaabab.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wakimbizi Dadaab

Baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakiishi katika kambi za Dadaab mashariki ya taifa hilo kwa zaidi ya miongo miwili.

Kenya imelishtumu kundi la Alshabaab kwa kujificha katika kambi hizo huku likiwasajili wanachama wapya.