Hillary Clinton kuwania urais Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hillary Clinton

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Hillary Clinton atakuwa rais bora na mwenye maono kwa nchi ya Marekani. Bi Clinton anatarajiwa kutangaza hii leo kuwa atawania uteuzi wa chama cha Democratic.

Obama amesema kuwa Bi Clinton alitekeleza kwa njia nzuri majukumu yake alipohudumu kama waziri wa mashauri ya kigeni. Atatangaza azma yake ya kuwania urais kwa njia ya video ambayo itasambazwa kupitia kwa mitandao ya kijamii.

Kinyume na miaka minane iliyopita Bi Clinton anatarajiwa kuangazia zaidi jinsi wapiga kura wataandikisha historia kwa kumchagua kuwa mwanamke wa kwanza rais wa Marekani.