Shambulizi lawaua wanajesi 3 wa Saudia

Image caption Saudia Arabia

Wizara ya ulinzi nchini Saudi Arabia inasema kuwa maafisa watatu wa kijeshi wa taifa hilo wameuawa na kombora lililofyatuliwa kwenda nchini humo na waasi wa Houthi kutoka nchini Yemen.

Taarifa rasmi ilisema kuwa kombora hilo lilianguka kwenye kituo kimoja cha kijeshi cha Najran nchini Saudi Arabia.

Shirika moja la habari nchini Saudi Arabia nalo lilisema kuwa waasi 500 wa Houthi wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi yanayoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen.