Madonna ambusu Drake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Madonna ametibua mjadala baada ya kumbusu Drake jukwaani

Mwanamuziki mkongwe Madonna amejijengea sifa ya kutokua muoga katika maswala ya ngono wala ya kijamii.

Lakini alichokifanya mwishoni mwa juma liliwaacha wengi vinywa wazi .

Bibi huyo mwenye umri wa miaka 56 alishindwa kustahimili mvuto wa mwanamuziki wa kizazi kipya Drake alipokuwa akimwaga misstari mbele ya mashabiki wake katika onyesho

la California Coachella.

Image caption Madonna ambusu Drake

Malkia huyo wa mziki wa ''POP'' alitua jukwaani Drake alipokuwa akiimba wimbo wake maarufu ''Madonna''

ilionekana kama aliyeshikwa na jazba baada ya kushuhudia wimbo wa ''Human Nature'' na ''Hung Up''

na akajipata jukwaani akampiga pambaja na kumkumbatia na mara akampiga busu.

Drake hakusema lolote wakati huo lakini alionekana kama aliyeshtuliwa sana na tukio hilo.

Image caption Drake baada ya kupigwa kubusu na Madonna

Picha zinaonesha alishikwa na kinyaa.

Ajabu nikuwa i Madonna alimpokonya kinasa sauti na kusema

"mimi ndiye Madonna" na akaondoka jukwaani.