Mamake Beyoncé Knowles,Tina 61, aolewa

Image caption Maharusi Tina na Richard Lawson

Mamake Beyonce Knowles,Tina 61,ameolewa kwa mara ya pili .

Tina aliolewa na mchumbake wa siku nyingi msanii Richard Lawson, mwenye umri wa miaka 67.

Wawili hao walifunga pingu za maisha katika boti moja la kifahari karibu na ufukwe wa Newport California.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanawe Beyonce na Solange walishuhudia ndoa hiyo

Beyoncé na mumewe Jay Z walikuwepo kushuhudia ndoa ya bi Tina.

Dadake Beyoncé Tina, Solange pia alikuwepo katika hafla hiyo ya kufana.

Mumewe Richard anakumbukwa kwa mchango wake katika riwaya ya ''All My Children'', iliyosimulia msiba wa mwaka wa 1982 wa Poltergeist.

Image caption Bwana na Bi Harusi Tina na Richard Lawson

Imekuwa ni msimu wa baraka kwa familia ya bi Tina ambaye majuzi tu alishuhudia ndoa ya mwanawe Solange na promota wa muziki Alan Ferguson mwisho wa mwaka uliopita.

Haijabainika iwapo baba yao mzazi ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa beyonce' bwana Mathew Knowles alikuwepo.

Image caption Tina na Mathew Knowles katika ndoa yao ya awali

Mathew, 63, aliishi na Tina kwa miaka 31 kati ya mwaka wa 1980 na 2011 na walijaaliwa watoto wawili Beyonce na Solange.

Baada ya wawili hao kutofautiana Mathew alimuoa bi Gena Charmaine mwaka wa 2013 huko Houston, Texas Marekani..