Uchina yalaumu Dalai Lama kwa fujo Tibet

Image caption Uchina imemlaumu kiongozi wa Tibet aliyeko uhamishoni Dalai Lama, kwa kutokuwa mwaaminifu

Kwa mara nyingine tena, Uchina imemlaumu kiongozi wa Tibet aliyeko uhamishoni Dalai Lama, kwa kutokuwa mwaaminifu na kushinikiza kiujanja uhuru wa watu wa Tibet.

China inadai kuwa kiongozi huyo amebadilisha mbinu badala ya kutaka kutambuliwa kwa jimbo hilo kama alivyokuwa akishinikiza hapo awali.

China imeanzisha makabiliano makali dhidi ya kiongozi wa kidini wa watu wa Tibet, Dalai Lama, na kumlaumu kwa kutumia ghasia kushunikiza uhuru wa Tibet.

Haki miliki ya picha AP
Image caption China imeanzisha makabiliano makali dhidi ya kiongozi huyo wa kidini wa watu wa Tibet

Katika taarifa ndefu inayoelezea mfumo mzima ya maoni ya jimbo la Himalaya, China inasema kuwa katika hali ilivyo sasa, hakuna haja kabisa ya kufanya mazungumzo na kinara huyo wa kidini aliye uhamishoni India.

Kwa muda mrefu Dalai Lama amekuwa akitetea uhuru wa kujitenga wa jimbo la Tibet, na alikuwa na matumaini makubwa kwa Rais wa sasa wa China, Xi Jinping, atatumia mbinu tofauti katika uhusiano naye na wa watu wa Tibet.

Taarifa hiyo pia ambayo ilichapishwa na shirika la habari la kitaifa la Xinhua, inasema kuwa wakuu mjini Beijing wanamuomba Dalai Lama kuweka kando ndoto yake ya hatma ya baadaye ya Tibet.

Image caption Dalai Lama ambaye amekuwa uhamishoni nchini India tangu mwaka 1959

Aidha China inamtaka akubali kuwa jimbo hilo limekuwa sehemu ya China kwa miaka na mikaka na kuwa hilo halitabadilika hivi karibuni.

Haijajulikana ni kwa nini taarifa hiyo ya kina imetolewa sasa.

Lakini waandishi habari mjini Beijing wamejitokeza hivi majuzi na kupinga maoni hayo ya Dalai Lama ambaye amekuwa uhamishoni nchini India tangu mwaka 1959.