Watu 5 zaidi wauawa Afrika Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wageni 5 zaidi wameuawa huko Durban

Watu watano zaidi wameuawa katika mashambulizi ya kibaguzi katika mji wa Durban nchini Africa Kusini.

Doria za maafisa wa polisi zimeimarishwa dhidi ya mashambulizi zaidi ya maduka yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya afrika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa kigeni wamekimbilia usalama katika vituo vya polisi

Wengi wamelazimika kuhamia katika makaazi ya mda ,huku Malawi ikiripoti kuwaondoa raia wake ambao wameachwa bila makao.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameshtumu mashambulizi hayo na kubuni kamati ya kujaribu kurejesha hali ya usalama.