Balozi wa mapenzi ya jinsia moja Vatican

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Balozi mteuzi Laurent Stefanini

Serikali ya Ufaransa imesema kuwa inangojea jibu kutoka kwa kanisa Katoliki kuhusu uajiri wa balozi wa mapenzi ya jinsia moja katika makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican.

Msemaji wa serikali hiyo amesema kuwa Ufaransa haitaondoa uteuzi wake wa Laurent Stefanini ambao ulifanywa mwezi Januari.

Waangalizi wanasema kuwa uteuzi wowote unaofanywa na kanisa katoliki huthibitishwa kati ya mda wa wiki sita na kwamba kimya hicho kikuu kinaamaanisha kwamba uteuzi huo umekataliwa.

Uteuzi huo unaonekana kama mtihani kwa upande wa Papa francis ambaye amekuwa na msimamo ulio huru kuhusiana na wapenzi wa jinsia moja.