IMF:Tishio la kuzorota kiuchumi lapanda

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Christine Lagarde

Shirika la Fedha Duniani (IMF) limesema kuwa hatari ya kuzorota kwa uchumi duniani imeongezeka.

Katika taarifa mpya, IMF linasema kuwa uchumi wa dunia umezongwa na bei duni za mafuta na kuporomoka kwa bei katika masoko ya hisa.

Ingawa bei ya chini ya mafuta imeimarisha ukuaji wa uchumi, masoko yanayoibuka kama vile Brazil, Nigeria na Venezuela yamezorota kwa sababu yanategemea mauzo ya mafuta katika uchumi wao.

Kupanda kwa Dola pia kunaletea kampuni matatizo hasa kwa wale waliokopa pesa kupitia sarafu hiyo ya dola ambazo watalipa kwa pesa zao wenyewe.