Nokia kununua Alcatel-Lucent

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nokia

Chini ya mkataba wa kununua hisa zote,wamiliki wa hisa za Alcatel-Lucent watamiliki asilimia 33.5 ya kampuni hiyo mpya huku wamiliki wa hisa za Nokia wakichukua asilimia 66.5.

Kampuni zote mbili zimesema kuwa wakurugenzi wake wamekubaliana ununuzi wa Alcatel-Lucent na wanatarajia mpango huo kuafikiwa katika nusu ya kwanza ya mwaka ujao.

Muungano huo utabuni kifaa cha mawasiliano barani Ulaya kitakachogharimu yuro billioni 40.

Mkuu wa kampuni ya Nokia Rajeev Suri amesema kuwa kampuni hiyo ilio na teknologia chungu nzima itawasaidia kuongeza ujuzi katika kila sehemu watakayochagua kushindana.

''Ninaamini kwamba huu ni mpango kabambe uliofanyika wakati mzuri.''