Zuma ashtumu ghasia za ubaguzi A Kusini

Image caption Rais Jacob Zuma

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ameshutumu ghasia zilizopo nchini humo hivi sasa ambapo wahamiaji wageni wameshambuliwa.

Ametaja ghasia hizo kama za kutisha na zisizokubalika.

Watu watano wameuawa tangu juma lililopita ambapo wamealaumiwa na wenyeji kwa kufanya kazi wanazostahili kufanya wao.

Akihutubia bunge leo alasiri, Rais Zuma alisema mashambulizi hayo yalikiuka haki za kibinadamu kama vile haki ya kuwa hai na kuheshimiwa.

Awali maelfu ya raia wa Afrika Kusini wamefanya maandamano katika mji wa Durban kulalamikia kile walichotaja kama ukatili dhidi ya Waafrika wengine.

Katika maeneo yanayopakana na Johannesburg, wenye maduka wenye asili ya kutoka Ethiopia, Somalia na maeneo mengine ya Afrika walifunga biashara zao, wakiogopa kuwa mali yao itaporwa.