Boko Haram lawaua watu 10 Cameroon

Haki miliki ya picha Other
Image caption Boko Haram lawaua watu 10 Cameroon

Takriban watu kumi wameuawa kazkazini mwa Cameroon katika shambulio baya lililotekelezwa na kundi la Boko Haram.

Jeshi la Cameroon linasema kuwa wapiganaji hao wa jihad walishambulia vijiji viwili kazkazini mwa Wilaya ya Kolofata hapo jana usiku.

Walivuka mpaka na kutorokea Nigeria kabla y kuwasili kwa majeshi ya Cameroon.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Cameroon wanaokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram

Kundi la Boko Haram mara kwa mara limefanya mashambulizi kazkazini mwa Cameroon.

Mbali na Cameroon, Boko haram pia limeshambulia mataifa ya Chad na Niger, ingawa mashambulio mengi yanatakekelezwa Nchini Nigeria.