Raia wa Burundi waandamana dhidi ya rais

Image caption Maandamano ya kumpinga rais wa Burundi Piere Nkurunziza yamefanyika mjini Bujumbura

Polisi nchini Burundi wamerusha mabomu ya kutoa machozi na maji, ili kuwatawanya mamia ya waandamanaji katika mji mkuu Bujumbura.

Maandamano hayo ni ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza, kutowania tena kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao, unaopangiwa kufanyika mwezi Juni.

Mwaandishi wa BBC mjini Bujumbura, anasema kuwa malori makubwa yanayobeba vitoa machozi yamewekwa tayari kukabiliana na waandamanaji hao kote katika mji huo.

Anasema kuwa wazazi wamekimbia shuleni ili kuwaondosha watoto wao na kuwapeleka nyumbani.

Bwana Nkurunziza hajasema hadharani iwapo atawania kiti cha urais kwa muhula mwingine, lakini kuna tetesi kuwa ana mpango wa kufanya hivyo.