Mapigano makali yaendelea Ramadi, Iraq

Haki miliki ya picha AP
Image caption Majeshi ya usalama yakiwasili mjini Ramadi kupambana dhidi ya wapiganaji wa Islamic State

Mapigano yanaendelea kuwania udhibiti wa mji wa Ramadi nchini Iraq kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa Islamic State.

Majeshi yanayoongozwa na Marekani yamefanya mashambulio ya anga dhidi ya vijiji vitatu ambavyo vilikuwa vimetwaliwa na majeshi ya Islamic State Jumatano.

Majeshi ya serikali ya Iraq mjini Ramadi pia yameripotiwa kupambana na wapiganaji wa I-S.

Maelfu ya watu wanakimbia mji wa Ramadi wakati huu mapiganao yanapopamba moto.

Kiongozi mmoja wa kisiasa wa eneo hilo Farhan Mohamed wa baraza la jimbo la Anbar ameishutumu serikali ya Iraq inayodhibitiwa na waumini wa madhehebu ya Kiislam ya Shia kwa kulitelekeza jimbo la Anbar wakati likiwa katika mapigano makubwa.

Jimbo la Anbar, wakazi wake wengi ni wa madhehebu ya Sunni.