Obama: mabadiliko ya hewa hayakanushiki

Mwanamme mbele ya moto Colorado, Marekani,  Juni 2013, Haki miliki ya picha AP

Rais Obama ameonya kuwa mabadiliko ya hali ya hewa hayawezi tena kukanushwa au kudharauliwa, na amesema ndio tishio kubwa kabisa linalokabili dunia.

Katika hotuba yake ya kila juma, Rais Obama alisema anataka aweze kuwatazama watoto na wajuukuu wake machoni na kusema kuwa kila liwezalo limefanywa kupambana na msukosuko huo.

Bwana Obama hivi karibuni aliahidi kupunguza sana kiwango cha gesi inayozidisha joto inayotolewa na Marekani - kiwango cha pili kikubwa kabisa duniani - kabla ya mkutano wa viongozi wa dunia mwezi wa Disemba.

Mipango yake inapingwa vikali na wanasiasa wengi wa chama cha Republican ambao wanadai kuwa itaumiza makampuni ya Marekani.