Saudia kutoa msaada unaohitajika Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yemen

Saudi Arabia, inayoongoza mashambulio ya ndege dhidi ya wapiganaji nchini Yemen, imeahidi kutoa idadi ya fedha ambayo Umoja wa Mataifa imesema inahitajika nchini Yemen.

Umoja wa Mataifa uliomba msaada huo wa kimataifa hapo jana, kwa shughuli za dharura za usaidizi nchini Yemen.

Shirika la habari la taifa la Saudi Arabia, linasema kuwa nchi hiyo itatoa dola laki mbili na 74 milioni, kama msaada wa kiutu kwa Wayemeni walioathirika na vita.

Haki miliki ya picha b
Image caption Yemen

Taarifa rasmi ilisema Saudi Arabia inasimama pamoja na ndugu zake wa Yemen.

Oparesheni inayoongozwa na Saudi Arabia, dhidi ya wapiganaji wa Houthi (na askari wanaopigana kwa niaba ya rais wa zamani, Ali Abdullah Saleh, ilianza wiki tatu zilizopita.

(Umoja wa Mataifa unasema mamia ya watu wamekufa, na maelfu ya familia zimekimbia makwao wakati vita vikizidi.)