Wazimbabwe wapinga ubaguzi Afrika kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa kigeni waandamani dhidi ya Ubaguzi dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini

Mamia ya raia wa Zimbambwe wameandamana nje ya ubalozi wa Afrika Kusini mjini Harare wakitaka kusitishwa kwa mashambulizi yanayoendeshwa dhidi ya wahamiaji nchini Afrika kusini.

Polisi wa kupambana na ghasia walitumwa waandamanaji hao walipojaribu kuharibu milango ya ubalozi huo.

Maelfu ya Wazimbabwe huishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini ambapo takriban watu watano wameuawa kwenye mashambulizi yanayowalenga wageni.

Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme wa zulu Goodwill Zwelethini kusema kuwa wageni ni lazima waondoke Afrika Kusini.