IS latoa video ya mauaji ya wakristo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption ISIS

Wanamgambo wa kundi la Islamic State wametoa kanda ya video wanayosema inaonyesha mauaji ya takriban Wakristo 30 kutoka Ethiopia waliokamatwa na washirika wa IS nchini Libya.

Picha za kundi moja zimeonyesha wakikatwa vichwa katika ufukwe wa bahari huku picha nyengine zikionyesha kundi jingine la raia hao wakipigwa risasi kichwani katika jangwa.

Maandishi katika kanda hiyo yanasema kuwa waathiriwa ni wanachama wa kanisa la Ethiopia.

Kanda hiyo ya dakika 29 inaonyesha alama ya kundi la mawasiliano la IS kwa jina Al-Furqan na inafanana na ile iliotolewa hapo awali na kundi hilo ikiwemo ile iliochapishwa mwezi Februari ambayo ilikuwa ikiwaonyesha wapiganaji wa kundi hilo wakiwakata vichwa wakristo 21 wa Misri katika ufukwe wa bahari nchini Libya.