Jaguar awakasirisha mashabiki Marekani

Image caption Msanii wa kenya Jaguar

Mwanamuziki wa Kenya Charles Njagua kanyi anayejulikana kama 'Jaguar' alitarajiwa kuwatumbuiza raia wa Atlanta nchini Marekani siku ya ijumaa lakini hakuonekana hadi asubuhi ya siku ya jumamosi na hivyobasi kuwawacha mashabiki wake wakisikitika.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, msanii huyo ambaye alitarajiwa kuanza kuwatumbuiza mashabiki hao mwendo wa saa nne usiku aliwasili katika jukwaa saa nane na nusu alfajiri wakati ambapo mashabiki walikuwa wanajiandaa kuondoka katika ukumbi wa AR Lounge katika barabara ya Farnklin huko Marietta ,Georgia.

Aliwatumbuiza kwa dakika 26 pekee kabla ya kuondoka.

Mashambiki waliojawa na ghadhabu walikasirishwa na waandalizi kwa kushindwa kuafikia muda uliowekwa.

''Tunataka kuwaambia wanamuziki wa Kenya kwamba hapa ni tofauti.hatutaki kujua wanavyoelewana na mashabiki wengine kwengine..hapa tunaheshimu wakati'', alise Joane Wambui ambaye aliondoka katika ukumbi huo saa moja kabla ya kuwasili kwa Jaguar.

''Ninafanya kazi asubuhi.nilikuwa nimepanga kumuona juaguar kufikia saa sita usiku lakini sasa nimesikitishwa aliiambia Nation katika ukumbu huo''.