Rinda lauzwa shilingi milioni 12 Marekani

Image caption Rida la O'hara katika filamu ya Gone with the wind lauzwa kwa kitita cha shilimi milioni 12

Rinda la Vivien Leigh aliyekuwa akiigiza kama Scarlet O'Hara mwaka 1939 katika filamu ya Gone With the Wind limeuzwa kwa kitita cha shilingi millioni 12.8 fedha za kenya ama dola 137,000.

Kulingana na kampuni ya mnada ya Heritage mjini Beverly Hill,jimbo la California rinda hilo liliuzwa mara mbili ya bei lililoanzia kuuzwa katika mnada.

'Gone with the wind' ni stori ya utunzi wa kitabu cha Margeret Mitchel ambacho kiliigizwa na kubuni filamu ilioshinda tuzo la Academy.

Rinda la O'Hara ni miongoni mwa vitu vya kumbukumbu vya filamu hiyo viivychukuliwa na James Tumblin msanii wa mapambo kutoka studio za Universal.