Ukraine:Waasi wadaiwa kukiuka mkataba

Haki miliki ya picha AP
Image caption wanajeshi wa Ukraine wakijiandaa kuwashambulia waasi

Serikali ya Ukraine inasema kuwa waasi wanaungwa mkono na Urusi wamekiuka pakubwa muafaka wa amani mara 20 zaidi.

Muafaka huo uliafikiwa kusitisha vita katika mji wa Donetsk ulioko mashariki mwa Ukraine.

Duru kutoka kusini mashariki mwa Ukraine, zinasema kuwa kumeshuhudiwa mapigano mapya kati ya wanajeshi waaminifu kwa serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Mapigano yamechacha katika kijiji cha Shyrokyne - kilichoko katika mji wa bandarini wa Mariupol.