Hospitali zaishiwa na madawa Yemen

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu waliojeruhiwa kwenye vita nchini Yemen

Hospitali kwenye mji wa bandari wa Yemen, Aden zinaishiwa na bidhaa muhimu za matibabu wakati mapigano kati ya vikosi vya seriali vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Shia wa Houthi yanapochacha.

Mwandishi wa bbc ambaye alizuru mji huo aliambiwa kuwa wagonjwa walikuwa wakifa kwa sababu hawangeweza kutibiwa kwa njia inayofaa.

Makundi ya kutoa huduma za matibabu yamelemewa na idadi ya wagonjwa wanaolazwa na yametoa wito kwa madawa zaidi na vifaa vingine vya matibau.

Kiongozi wa waasi amekashifu Saudi Arabia kwa kujaribu kuivamia na kuiteka nchi ya Yemen.