Msanii jela kwa kukejeli bendera- Misri

Haki miliki ya picha e
Image caption Bendera ya Misri

Msanii mmoja wa kucheza dansi , raia wa Armenia nchini Misri, amehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani, kwa madai ya kutusi bendera ya taifa hilo.

Msanii huyo anayefahamika kama Safinas, alihukumiwa kwa kosa la kuvaa sare iliyofanana na bendera ya Mirsi katika hoteli moja ya kifahari iliyoko karibu bahari ya Shamu.

Lakini mawakili wake wamesema msanii huyo hakunuia kukejeli bendera hiyo.

Tangu mwaka uliopita, kuonyesha dharua ya aina yoyote kwa bendera ya taifa ni kosa ambalo adhabu yake ni kifungo cha hadi mwaka mmoja gerezani.