Wafuasi wa Muslim Brotherhood kunyongwa

Haki miliki ya picha none
Image caption Wafuasi wa Muslim Brotherhood

Mahakama moja Nchini Misri, imewahukumu kifo zaidi ya wanachama 20 wa vugu vugu la Muslim Brotherhood, kutokana na shambulio lililolenga kituo cha polisi, baada ya kuondolewa mamlakani kwa rais Mohamed Morsi, mnamo mwaka wa 2013.

Wanachama 20 wa kundi hilo lililoharamishwa, walipatikana na hatia ya mauwaji na jaribio la kukusudia kuuwa, wakati wa shambulio kwenye kituo cha polisi, lililosababisha kifo cha askari mmoja.

Maelfu ya wanachama wa kundi hilo la Muslim Brotherhood na washirika wao, wamehukumiwa kifo na maelfu ya wengine wanatumikia hukumu ya muda mrefu jela kama kampeini ya serikali ya rais Abdul Fattah al-Sisi, ya kulisambaratisha kundi hilo.