Pembe za Ndovu zanaswa Thailand

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shehena ya pembe za Ndovu

Maafisa wakuu wa idara ya forodha nchini Thailand, wanasema kuwa wamenasa shehena kubwa zaidi ya pembe za ndovu kuwahi kunaswa katika historia ya taifa hilo.

Wanasema kuwa wamefuatilia chimbuko la shehena hiyo yenye uzito wa tani nne ya pembe za ndovu na kubaini zilitoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Maafisa hao wanasema kuwa pembe hiyo inayogharimu dola milioni sita ilikuwa njiani kwenda mjini Laos, ambako inaaminika ingeuzwa kwa wateja nchini Thailand, China au Vietnam.

Thailand inakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi kuhusu namna inavyozembea katika kukabiliana na bidhaa za wanyama pori zinazouzwa nje ya Nchi hiyo, iwapo haitafanya lolote kuzuia biashara hiyo haramu ya pembe za ndovu.