Ajali;Watalii 12 waangamia Nepal

Haki miliki ya picha NEPAL ARMED FORCE
Image caption Eneo kulikotokea ajali ya basi

Watalii kumi na wawili kutoka nchini Indian wameaga dunia kufuatia ajali ya basi walilokuwa wakisafiria katika wilaya ya Dhading karibu na mji wa Kathmandu nchini Nepal.

Basi hilo lilikuwa likitoka kathmandu kwenda mji wa Gorakhpur.

Kati ya wale waliokufa ni pamoja na wanawake saba. Watu wengine thelathini walijeruhiwa.

Kulingana na mkuu wa wilaya Basudev Ghimire ni kuwa basi hilo , lilipoteza mwelekeo na kupingirika chini umbali wa mita 150 kutoka barabarani.

Ahalia hiyo ilitokea mapema leo Jumatano.