Meningitis; Shule zafungwa Niger

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanafunzi wakiwa shuleni

Shule zote nchini Niger zinafungwa kwa siku kadha wakati nchi hiyo inapojaribu kukabilian na mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo au meningitis, ambao umewaua zaidi ya watu 80 mwaka huu.

Waziri mkuu Brigi Rafini amezindua shughuli ya kutoa chanjo kwa watoto wote kati ya miaka mwili na kumi na tano, lakini akasema kuwa Niger ina nusu tu ya madawa yanayohitajika ambapo alitoa wito kwa shirika la afya duniani WHO kwa msaada zaidi.

Waziri wa afya nchini humo amewaonya watu akiwataka kuacha kutumia madawa yasiyoidhinishwa akisema kuwa dawa hizo zinaweza kuwa za aina tofauti ya ugonjwa huo.

Asilimia kubwa ya visa 900 vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa vimekuwa mji mkuu Niamey na magharibi mwa nchi.