Mashambulizi yaanza tena Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege ya Saudi Arabia yaenda kushambulia Yemen

Muungano unaongozwa na Saudi Arabia umerejelea tena mashambulizi ya angani dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen huku pia kukiendelea mapigano ya ardhini.

Kuanza tena kwa mashambulizi hayo kunakuja saa kadhaa baada ya Saudi Arabia kutangaza kuwa mashambulizi hayo yamefanikiwa na kwamba yalikuwa yanafika mwisho.

Mashambulizi hayo yalianza baada ya waasi kuteka makao makuu ya jeshi kwenye mji wa Taez.

Licha ya hili habari zinasema kuwa makubaliano yanatarajiwa kuwepo na waasi hao.