Makao ya kiongozi wa upinzani yazungukwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Sudan Kusini

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini Lam Akol anasema kuwa nyumba yake imezingirwa na vikosi vya usalama na sasa yuko chini ya kuzuizi cha nyumbani.

Bwana Akol ambaye ni kiongozi wa Sudan People's Liberation Movement - Democratic Change, aliiambia BBC kuwa alikuwa amewasiliana na serikali ya Salva Kiir kuuliza ni kwa nini hatua hizo zimechukuliwa , lakini licha ya hilo bado hajapata jibu.

Image caption Lam Akol

Siku za hivi majuzi bwana Akol amekuwa akiilaumu vikali serikali ya Sudan Kusini kutokana na mipango ya kutaka kutumia karibu dola milioni mia mbili kwenye sherehe za kuadhimisha miaka minne ya uhuru wakati ambapo hali ya uchumi ni mbaya.