Kijana aliyewavamia polisi auawa Israel

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa polisi wa Israel

Polisi nchini Israeli wanasema kuwa wamemuua kwa kumpiga risasi kijana mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa na kisu kwenye kizuizi kimoja mashariki mwa Jerusalem.

Wanasema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 alijaribu kuwadunga kisu maafisa wa mpakani alipokuwa akiwavamia maafisa hao na kisu mkononi.

Kisa hicho kilitokea mapema jumamosi karibu na kizuizi cha Al-Zaim

Polisi wa Isreali walichapisha mitandaoni picha na kisu ambacho kijana hiyo alikuwa nacho.