Tetemeko la ardhi lawaua 1000 Nepal

Haki miliki ya picha EPA
Image caption tetemekonla ardhi mjini Nepal

Zaidi ya watu elfu moja wamepoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal karibu na mji mkuu wa Kathmandu.

Polisi wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakishindwa kujulikana walipo kwa hofu huenda wamefukiwa na kifusi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Tetemeko la ardhi mjni Nepal lenye vipimo vya richa 9.7

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa saba nukta tisa katika vipimo vya richa limeathiri maeneo ya katikati mwa mji wa Kathmandu na mji wa Pokhara.

Majengo kadhaa ya kihistoria yamevunjwa na tetemeko hilo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Tetemeko la ardhi Nepal

Serikali imetangaza hali ya dharura huku ikisema inahitaji msaada wa kimataifa.