Raia wa Togo wapiga kura

Image caption Raia wa Togo wapiga kura kumchagua raia mpya

Uchaguzi wa urais unaendelea nchini Togo huku rais wa sasa Faure Gnassingbé akigombea muhula wa tatu.

Mgombea wa upinzani Jean-Pierre Fabre ametaka kuwepo mabadiliko kando na familia ya Gnassingbé ambayo imekuwa madarakani kwa miaka 48.

Faure Gnassingbé amekuwa madarakani tangu babake Gnassingbé Eyadema, aage dunia baada ya kuchukua mamlaka mwaka 1967.