Watu 2 wauawa katika maandamano Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Ghasia zazuka nchini Burundi

Watu wawili wameripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi kufuatia ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Bujumbura nchini Burundi.

Waandamanaji wameishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba baada ya uteuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu.

Image caption Maandamano Burundi

Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakikamatwa.

Maafisa wa polisi walikivamia kituo kimoja cha redio kinachounga mkono upinzani na kutishia kukifunga iwapo hakitasitisha matangazo yake ya moja kwa moja kuhusu maandamano hayo.