Uchaguzi wa urais waendelea Kazakhstan

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev

Watu nchini kazakhstan wameanza kupigia kura kweye uchaguzi wa mapema wa kumchagua rais.

Kura hiyo inatarajiwa kuongeza uongozi wa miaka 26 wa rais Nursultan Nazarbayev kwa miaka mingine mitano.

Vyama vya upinzani hivijakuwa na wagombea. Rais Nazarbayev amekuwa akifanya kampeni akiahidi kuboresha uchumi na masuala ya kijamii katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Makundi ya haki za bidamu yanaishutumu serikali kwa kuukandamiza upinzani.

Kazakhstan ina watu wenye asili ya Urusi na ghasia zilizotokea nchini Ukrain zilizua hofu kuwa watu wa asili ya Urusi wanaweza kuwa na ajenda sawa na iliyo nchini Ukrain.