Wanaharakati wafanya maandamano Burundi

Image caption Raia wa Burundi wanaotoroka ghasia nchini mwao

Wanaharakati wa upinzani nchini Burundi wameingia mitaani kwa siku ya pili kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu .

Polisi walivunja maandamano hayo.

Waandamanaji kadha walipigwa risasi jana Jumapili.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 15,000 wameitoroka Burundi Congo kutokana na hofu kuwa huenda kukatokea ghasia kabla ya uchaguzi wa mwezi Juni.