Mazungumzo:Waasi wapewa masharti Yemen

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waasi wa Shia wanaojulikana kama Houthi

Huku mapigano yakiendelea kote nchini Yemen waziri wa mashauri ya kigeni wa nchi hiyo aliye uhamishoni ameiambia BBC kuwa serikali yake imejiandaa kwa mazungumza ya amani na waasi wa shia wa Houthi ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Riyadh Yaseen ambaye ni mmoja wa watu walioomba hifadhi nchini Saudi Arabia anasema kuwa waasi wa Houthi ni lazima kwanza waweke silaha zao chini na kutangaza kuwa wao si wanamgambo bali chama cha kisiasa.

Alisema kuwa hakutakuwa na mazungumzo na kiongozi wa waasi Abdul Malik al-Houthi, na pia rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.