Rais Omar al Bashir ashinda uchaguzi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Omar Al Bashir

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amechaguliwa kwa muhula mwengine wa miaka mitano kuendelea kuiongoza nchi hiyo.

Omar al-Bashir ameitawala Sudan kwa zaidi ya miaka 26 sasa.

Ameshinda uchaguzi wa sasa kwa zaidi ya asilimia 95 kwani wapinzani wake walisusia wakisema uchaguzi huo haungekuwa huru na wa haki - kauli inayoungwa mkono na mataifa ya Ulaya.

Image caption Sudan

Rais Bashir angali anakabiliwa na agizo la kukamatwa na koti ya kimataifa ICC inayomtuhumu kuhusika katika mauaji ya kimbari huko Dafur.

Baada ya uchaguzi huu ameahidi kutatua matatizo yanayowakumba raia wa Sudan ikiwemo matatizo ya kiuchumi na kisiasa yanayokumba taifa hilo.