Ni makosa kuwatengeza nyusi wanaume Iran

Image caption Iran

Wasusi nchini Iran wameonywa kutowatengeza wanaume nyusi zao.

Muungano wa wasusi nchini humo umewaambia wanachama wake kwamba unyoaji wa nyusi za wanaume ni kinyume na sheria za kiislamu.

Vilevile umewaambia wasusi kutowawekea tatoo wanaume .

Mamlaka nchini Iran imejaribu kuwazuia wanaume kufanyiwa urembo ikisema kuwa ni tamaduni za kimagharibi,lakini imeshindwa kuzuia ongezeko la wanaume wa taifa hilo ambao wanafahamu fesheni.