Raia wa Burundi wakiwa mtaani,kuonesha nguvu ya umma.
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania inaufuatilia mgogoro wa Burundi

Maandamano yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa siku ya tatu kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.

Watu wanachoma magurudumu ya magari na kuweka vizuizi huku nao polisi wakirusha vitoa machozi.

Maandamano hayo kwa mara ya kwanza, yamesambaa kwenda nje ya mji mkuu. Polisi wamezuia wanafunzi wa chuo kikuu kwenye mji ulio kati kati mwa nchi wa Gitega waliojaribu kuandamana kwenda mjini.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu 25,000 wamekimbia nchi hiyo ndani ya majuma mawili yaliyopita, wakihofia kuongezeka kwa ghasia kabla ya uchaguzi mkuu unaokuja.

Tanzania inao ushawishi mkubwa katika siasa za Burundi,kama utakumbuka mkataba wa amani wa Arusha, pia juhudi za baba wa Taifa la Tanzania Julius Kambarage Nyerere aliihangaikia sana Burundi irejee kwenye amani, je mgogoro wa Burundi Tanzania inauangaliaje? mwandishi wa BBC, aliyeko Dar-Es-Salaam Regina mziwanda amezungumza na msemaji wa serikali ya Tanzania Assah Mwambene.